Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igalula na Tabora Kaskazini, anawatangazia wananchi wote kuwa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaweka Wazi Daftri la Awali la Wapiga Kura kwa siku NNE kuanzia Tarehe 17-20/06/2020 kwenye vituo vyote vilivyotumika Wakati wa Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Uwekaji wazi huu utafanyika kwa kuzingatia tahadhari zote za afya kuhusu kuzuia maambukizi ya ugonjwawa COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.
***ZOEZI HILI LITAHUSU:-
1.Wapiga Kura wote walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015, walioandikishwa wakati wa Uboreshajiwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza na ya Pili kwa Mwaka 2019/2020.
2.Wapiga Kura hawa ni wale ambao hawakuhakiki taarifa zao wakati wa uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
3.Wapiga kura watakaohakiki taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura lilipowekwa wazi na kukuta picha zao hazipo wanatakiwa kwenda kwenye ofisi za Halimashauri ya UYUI eneo la GODAUNI Kijiji cha ILALWANSIMBA, ili wapigwe picha nyingine na kupewa kadi.
***UTARATIBU WA UHAKIKI***
Mpiga kura anaweza kuhakiki taarifa zake kwa njia zifuatazo:-
1.Mpiga Kura mwenyewe kufika katika kituo alichojiandikisha na kuhakiki taarifa zake katika orodha itakayokuwa imebandikwa katika kituo hicho. Mtu mmoja kwenye familia anaweza kukagua taarifa za familia nzima.
2.Mpiga Kura kupitia simu yake ya kiganjani kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo yatakayomwezesha kuhakiki taarifa zake.
3.Mpiga kura kupiga simu namba 0800112100 na kufuata maelekezo yatakayomwezesha kuhakiki taarifa zake.
4.Mpiga Kura kuhakiki taarifa zake kupitia Tovuti ya Tume, www.nec.go.tz kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa uhakiki na kuendelea kufuata maelekezo.
**MAMBO YA KUZINGATIA:-
1.Daftari la awali la wapiga kura litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha wapiga kura.
2.Iwapo mpiga Kura amehakiki taarifa zake kwa kutumia njia yoyote kati ya hizo nne na kutaka kufanya marekebisho ya taarifa zake atatakiwa kwenda katika Ofisiza Halmashauri ya UYUI Kijiji cha ILALWANSIMBA eneo la GODAUNI na kufanya marekebisho hayo.
3.Mpiga Kura anayehitaji kumuwekea pingamizi Mpiga Kura asiye na sifa zakuwemo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura ataenda katika Kituo kilicho pangwa kwenye Halmashauri husika.
4.Wapiga kura wanatakiwa kutoa taarifa za ndugu waliofariki dunia ili waondolewe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
*****Katika zoezi hili hakutakuwa na Uandikishaji wa Wapiga Kura Wapya. Aidha, hakutakuwa na Uboreshaji wa Taarifa za Wapiga Kura waliohama maeneo yao ya kiuchaguzi, waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika****.
**ZOEZI HILI NI LA SIKU NNE TUU, ZINGATIA MUDA**
*KUMBUKA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA, KWA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA UWAPO KITUONI*
Fuata maelekezo utakayopewa kituoni ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Corona.
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: +255 766616985
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.