NA TIGANYA VINCENT,
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Idete iliyopo Wilayani Uyui John Paul Mdaki na Kamati yake ya Ujenzi imepongezwa na Viongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa matumizi mazuri ya shilingi milioni 40 yaliweza kujenga na kukamilisha madarasa mawili.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi kwa niaba ya wenzake baada ya kukagua mradi huo na kuridhishwa na viwango vya ujenzi.
Amesema Mwalimu huyo na Kamati yake wameonyesha uzalendo mkubwa kwa kuweza kutumia milioni 36 kujenga madarasa mawili na kuweka samani kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi 80 na walimu wawili wakati wa vipindi.
Luteni Josephine ameongeza kuwa Mwenge wa Uhuru sio tu unakosoa pia unasifia pale Watendaji wamapofanya vizuri kwenye miradi ya umma na kuwataka watumishi wengine kuiga mfano wa Kamati ya Ujenzi ya shule ya Sekondari Idete,
“Mkuu wa Wilaya unaonaje kazi hii na Mwalimu Mkuu alivyo kwa kweli huyo anastahili kupandishwa na kuwa Afisa Elimu kwa kazi yake nzuri”amesisitiza,
Awali Afisa Elimu Sekondari , Ndg Jacob Makala amesema kuwa hadi kukamilika kwa kazi zote wametumia jumla ya Shilingi milioni 36.9 na kubaki na kiasi cha milioni 3.
Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuweka Msingi jumla ya miradi sita yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.
Wakati huo huo Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanapeleka maji safi na salama yaliyopo katika mtandao wa Ziwa Victoria katika Josho la Kijiji cha Kinyamwe ili wafugaji wawe na uhakika wa maji kwa ajili ya Josho lao.
Amesema mtandao wa maji ya ziwa Victoria uko karibu sana na Josho lao ni vema wakapelekewa maji hayo na kuachana na maji ambayo hayana uhakika,
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori amesema kati ya fedha hizo Serikali Kuu ni shilingi bilioni 2.2, Halmashauri ni milioni 223.6, michango ya wananchi milioni 297.3 na wadau wa maendeleo ni milioni 25.
Amesema mradi wa kwanza unahusu ufugaji wa nyuki katika Msitu wa Hifadhi wa Simbo ambao umegharimu milioni 58.2 na unaosimamiwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki cha Tabora.
Makori ametaja mradi mwingine uliotembelewa na Mwenge wa Uhuru ni ule wa shughuli za uogeshaji wa mifugo kwenye Josho la Kijiji cha Kinyamwe ambao umegharimu milioni 898.
Ameongeza kuwa mradi mwingine ni ule wa uwekezaji wa sekta binafsi katika ujenzi wa majengo ya biashara katika eneo la Isikizya ambao hadi kukamika utagharimu milioni 290.
Makori amesema Mwenge wa Uhuru umetembelea Hospitali ya Wilaya ya Uyui kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi na ujenzi wa mfumo wa ukusanyaji taarifa za utoaji wa huduma za afya ambapo kazi zote zimegharmu bilioni 2.3 hadi hivi sasa.
Amesema Mwenge wa Uhuru pia umetoa zawadi kwa Msindi wa Kwanza hadi wa Tatu wa mashindano wa mpira wa miguu kwa wanaume ya Jimbo la Igalula ambayo yamegharimu milioni 25.
Mwisho
Maelezo katika Picha.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa uhuru Luteni Josephine Mwambashi akiweka Jiwe la Msingi leo uzinduzi wa Madarasa ya Sekondari ya Idete iliyopo Wilyani Uyui
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 766616985
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.