• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali Yanayoulizwa Maranyingi |
    • Barua pepe za Watumishi |
Uyui  District Council
Uyui  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Kimsingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Administration and Human Resource
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Envinment and Sanitation
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Ugavi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za baraza la madiwani
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
      • Ratiba ya Mwekekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Hotuba Mbalimbali

Ufugaji Nyuki

1.0 UTANGULIZI:
Ufugaji wa nyuki unafanyika kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi, 1998, Sheria ya Ufugaji Nyuki Na. 15 ya mwaka 2002 na Kanuni za Ufugaji Nyuki, 2005. Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi, 1998 imelenga mambo makuu matatu ambayo ni:- (i) kukuza uchumi wa taifa (ii) kuhifadhi mazingira (iii) manufaa ya kijamii.

2.0 FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

  1. Nyuki hawahitaji uangalizi wa kila siku, ufugaji nyuki hauhitaji mtaji mkubwa na mapato    yatokanayo na shughuli hii hupatikana katika muda mfupi;
  2. Nyuki hukusanya chakula chao kwenye maua ya mimea ya asili  na iliyopandwa;
  3. Ufugaji nyuki hauhitaji ardhi yenye rutuba, mizinga ya nyuki inaweza kutundikwa kwenye eneo lisilofaa kwa kilimo kwani nyuki wanaweza kuruka umbali wa maili mbili kutafuta chakula;
  4. Ufugaji nyuki unaweza kufanywa na wanaume na wanawake wa rika zote;
  5. Ufugaji nyuki ni fursa kwa kujianzishia shughuli ya kujiajiri mwenyewe, huchangia katika usalama wa akiba ya chakula katika kaya kwa kuzalisha na kuuza mazao ya nyuki (asali na nta). Asali ni chakula bora chenye virutubisho kama wanga, protini, vitamini na madini; nta ni zao la biashara;
  6. Ufugaji nyuki uongeza wingi na ubora wa matunda na mbegu za mimea ya kupandwa mashambani na misitu ya asili kutokana na uchavushaji; ni muhimu katika kilimo endelevu, kuhifadhi  mazingira, kutunza ikolojia na kuboresha bioanuwai.

3.0 MAJUKUMU YA KITENGO CHA UFUGAJI NYUKI

  • Kuhakikisha wafugaji wa nyuki wanapata elimu juu ya ufugaji bora na teknolojia mpya za uzalishaji asali na nta.
  • Kuelimisha wafugaji juu ya uchakataji, ufungashaji na biashara ya mazao ya nyuki.
  • Kusimamia Sera, Sheria na Kanuni za ufugaji nyuki.
  • Kukusanya takwimu za uzalishaji wa mazao ya nyuki na kuandaa taarifa za utekelezaji.

3.1  Elimu inayotolewa
Elimu inayotolewa inahusu yafuatayo:-              
    (i) Nyuki na tabia zake
    (ii) Matumizi ya zana za ufugaji nyuki
    (iii) Uanzishaji na usimamizi wa manzuki
   (iv) Mizinga ya nyuki ya kisasa
   (v) Uambikaji,utundikaji na ukamataji wa makundi ya nyuki
   (vi) Uangalizi wa makundi
   (vii) Mazao ya nyuki
   (viii) Maadui wa nyuki na njia za kuwakabili
   (ix) Uchakataji na ufungashaji asali na nta
   (x) Sera, sheria na kanuni za ufugaji nyuki
   (xi) Elimu ya ujasiliamali

4.0 IDADI YA WAFUGAJI
Baadhi ya wananchi katika Kata 30  hujishughulisha na shughuli za  ufugaji nyuki kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini.

Jedwali Na. 1

Mwaka 
Idadi ya mizinga
Idadi ya wafugaji
Idadi ya uzalishaji
Ya magogo
Ya magome
Ya kisasa
Me 
Ke 
Jumla 
Asali kgs
Thamani Tshs.
Nta kgs 
Tahamani Tshs.
2014/15
486,487
21,105
2,465
11,860
238
12,098
35,160
87,900,000
11,590
104,310,000
2015/16
487,717
20,683
2,515
12,175
325
12,445
50,700
152,100,000
21,304
234,388,000
2016/17
488,936
20,170
2,860
12,253
343
12,541
40,350
148,084,506
5,475
65,700,000


lifuatalo ni jedwali linaloonyesha idadi ya hifadhi za nyuki, vyama vya msingi vya ushirika wa wafugaji na vikundi vya nyuki.

Jedwali No. 2

Idadi ya hifadhi za nyuki
Idadi ya vyama vya msingi vya Ushirika vya ufugaji Nyuki
Idadi ya vikundi ya ufugaji Nyuki

25

4

28


Kuunda kikundi:Unatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
 (i)  Kikundi kiwe na katiba.
(ii)  Kikundi kisajiliwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (wasiliana na Afisa Mtendaji kuhusu taratibu za kusajili kikundi).
(iii) Wanakikundi wawe tayari kupewa mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki na ujasiliamali.       Mafunzo yatatolewa kwa siku na muda  mtakaokubaliana na wataalam.
Ufugaji binafsi au kikundi kuanzishwa inabidi kuzingatia sana uwepo wa eneo la kufugia (Manzuki) .

5.0 MANZUKI
Eneo maalumu au shamba linalotumika kuhifadhi makundi ya nyuki yaliyopo ndani ya mizinga kwa malengo ya kuzalisha mazao ya nyuki.

Sifa za manzuki:
Eneo lifaalo kwa shughuli za ufugaji nyuki ni lazima liwe na sifa zifuatazo:

  1. Miti, uoto wowote wa asili na mimea mbalimbali / Ufahamu juu ya miti ya nyuki (yaani miti ambayo nyuki hupata chakula) ni jambo la muhimu sana. Eneo liwe na mimea  inayotoa chakula mwaka mzima au kipindi fulani cha mwaka. Si lazima liwe shamba kubwa; bali hata eneo dogo linalozungukwa na miti itoayo chakula. Umbali wa miti na shamba usizidi km 2. Eneo hili linaweza kuongezewa chakula cha  nyuki kwa kupanda miti zaidi inayotoa maua au hata mazao ya kilimo yanayotoa maua.
  2. Chanzo cha maji ni vizuri kikawa cha kudumu, lakini kama cha kudumu hakipo basi maji yanaweza kupelekwa kwenye manzuki wakati wa ukame. Nyuki huyatumia maji kupoza joto ndani ya mzinga, kulainisha chakula na kulekebisha utamu wa asali ambayo hulishwa majana.
  3. Eneo la manzuki ni lazima liwe salama, mizinga, mazao yake, mifugo, binadamu, na mahali ambapo maadui wa nyuki hawezi kufikia makundi yako na kuyaharibu lakini pia ni vyema kuhakikisha kwamba maadui wa nyuki wanadhibitiwa. Usalama wa wakazi na wadau wengine pia lazima utiliwe maanani, Manzuki inatakiwa iwe mbali na maeneo wanayotumia watu kama masoko, mashule, zahanati, hospitali, barabara kuu na visima vya maji.
  4. Makundi ya nyuki yanahitaji kivuli cha kadri na kinga ya upepo ili hali ya kupunguza joto ndani ya mzinga.
    V.Eneo la manzuki ni vyema liwe linafikika kwa urahisi wakati wote ili kurahisisha uhudumiaji wa makundi ya nyuki pamoja na kufikisha mazao yake sokoni.


Matangazo

  • TANGAZO LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA April 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MKATABA April 18, 2024
  • TANGAZO LA MKOPO KWA UMMA October 04, 2024
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA KATIKA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) 2024 September 06, 2024
  • Soma zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA TABORA KATIKA WILAYA YA UYUI TAREHE 6 JANUARI 2024

    January 06, 2025
  • MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 26 SEPTEMBA 2024

    September 27, 2024
  • UYUI DC YAFANYA DUA NA SALA MAALUM KWA NCHI NA VIONGOZI WA NCHI KUELEKEA MAAZIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

    April 22, 2024
  • MHE. ZAKARIA MWANSANSU MKUU WA WILAYA YA UYUI AKISISITIZA MAMBO MUHIMU KATIKA KUELEKEA KUAZIMISHA MUUNGANO WA MIAKA 60 WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

    April 19, 2024
  • Soma zote

Video

SAMIA SULUH
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari Mpya

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Tabora RAS
  • Tovuti ya Baraza la Mitihani
  • Watumishi Portal
  • Tabora MC

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Uyui District Council

    Anuani ya Posta: S.L.P 610

    Simu ya Mezani: +255 26 296 6008

    Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886

    Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali Yanayoulizwa Maranyingi
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.